• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sharapova atolewa kwenye michezo ya Tennis ya wazi ya Ufaransa

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:03:38
    Kwenye tennis mwanadada Garbine Mugurunza amemchapa Maria Sharapova kwa seti 6-2, 6-1 na kuingia nusu fainali ya michezo ya tennis ya French Open. Hiki ni kipigo kitakatifu kwa Sharapova katika kipindi cha miaka sita. Kipigo hivi kimefurumua mengine ambayo yalikuwa hayajulikani kwa wengi katika medani ya tennis, ambayo yamo kwenye kitabu cha "unstoppable" kilichoandikiwa na Sharapova, kuwa Serena Williams anamchukia, kwa kuwa "ni msichana kimbaumbau aliyewahi kumshinda kwenye michezo ya wazi ya Ufaransa bila kutegemewa na wengi". Sharapova amesema kwenye kitabu hicho licha ya kuitwa kimbaumbau, Serena pia alisema baada ya kipigo alichopata mwaka 2004, kuwa hawezi tena kushindwa kwa huyo "changu". Na kweli tangu wakati huo, Serena hajawahi kushindwa dhidi ya Sharapova. Lakini wiki iliyopita baada ya ushindi Serena alikaribia kukutana na Sharapoava,l lakini alijitoa kutokana na alichokiita maumivu. Hata hivyo Serena mwenyewe amesema mengi ya yanayosemwa kwenye kitabu cha Sharapova ni umbea kwa asilimia 100.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako