Paundi elfu 5 za Nwanko Kanu zilizoibiwa uwanja wa ndege Russia zapatikana
(GMT+08:00) 2018-06-07 09:04:36
Wakati mashabiki, timu na maofisa wameanza kumiminika Russia kwa ajili ya kombe la dunia, ujia wa baadhi ya wageni haujawa rahisi baada ya kukumbana na matukio ya uhalifu. Mwanasoka Nwanko Kanu wa Nigeria amekuwa mhanga wa kwanza baada ya kuibiwa kitita cha paundi elfu 5, ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 15, alizokuwa ameweka kwenye begi lake akitokea nyumbani kwao Uingereza. Lakini kutokana na umakini wa wana usalama wa Russia wezi waliokuwa ni wafanyakazi wa uwanja wa ndege, wamekamatwa Kanu amerudishiwa pesa zake, na wahalifu wanakabiliwa na kifungo cha miaka sita gerezani.