• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya kutoza ushuru bidhaa za Marekani kuanzia Julai

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:30:05

    Kamati ya Ulaya imesema Umoja wa Ulaya utatoza ushuru dhidi ya bidhaa za Marekani kuanzia mwezi Julai, ikiwa ni moja ya hatua za kuijibu Marekani kutoza ushuru dhidi ya bidhaa za chuma cha pua na alumini kutoka Ulaya. Kamishna wa biashara wa Umoja wa Ulaya Bibi Cecilia Malmstrom amesema hii ni hatua madhubuti na yenye uwiano kujibu uamuzi haramu na wa upande mmoja uliotolewa na Marekani, kutoza ushuru dhidi ya bidhaa za chuma cha pua na alumini kutoka Ulaya kuanzia Juni mosi, na kusisitiza kuwa hatua hiyo inalingana na sheria ya biashara ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako