• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Iraq laidhinisha kuhesabiwa upya kwa kura zote za Uchaguzi wa wabunge

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:30:24

    Bunge la Iraq limeidhinisha kuhesabiwa upya kwa kura katika vituo vyote vya kupigia kura nchini kote, kutokana na tuhuma za udanganyifu na ukiukaji wa kanuni kwenye uchaguzi wa wabunge uliofanyika Mei 12. Kwenye kikao cha dharura, bunge hilo pia limepitisha uamuzi wa kuwasimamisha kazi maofisa tisa waandamizi wa Tume ya uchaguzi ya Iraq, na kuwateua majaji tisa kuchukua nyadhifa zao ili kusimamia utendaji wa tume hiyo. Maamuzi hayo ya bunge huenda yatabadilisha matokeo ya uchaguzi wa wabunge na kuahirisha uundaji wa serikali mpya ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako