• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini lakanusha habari kuwa linaandaa muswada wa sheria ya kutwaa ardhi inayomilikiwa na wageni

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:48:38

    Bunge la Afrika Kusini limekanusha uvumi kuwa linaandaa muswada wa sheria ya kutwaa ardhi inayomilikiwa na wageni nchini humo.

    Mwenyekiti mwenza wa kamati ya pamoja ya mapitio ya katiba ya bunge la Afrika Bw. Lewis Nzimande amesema serikali ya Afrika Kusini haiwalengi wageni, na habari hiyo ni uongo na inaweza kuwakatisha tamaa wawekezaji wageni.

    Bw. Nzimande amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia ujumbe unaoenezwa kwa njia ya Whatsapp, kuwa wageni wanaomiliki viwanja, wanaweza kuathiriwa na sheria hiyo.

    Bunge la taifa na mabaraza ya majimbo yameiagiza kamati hiyo kupendekeza mabadiliko ya lazima kwenye katiba, inapowezekana, kuhusu utaratibu wa muda wa kumiliki ardhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako