• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zambia yahakikisha inafanya mjadala kuhusu sheria ya usalama mtandaoni

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:59:06

    Serikali ya Zambia imesema wadau watakuwa na nafasi ya kushiriki kwenye utungaji wa sheria kuhusu usimamizi wa mitandao ya kijamii.

    Wiki hii kundi la wadau wa mtandao wa Internet wameitaka serikali isitishe mipango ya kuwasilisha bungeni mswada wa marekebisho ya kusimamia mitandao ya kijamii kuruhusu majadiliano zaidi.

    Wadau hao wanaona si haki kwa serikali kuendelea na mswada huo bila kuwashirikisha wadau. Hata hivyo msemaji mkuu wa serikali ya Zambia Bibi Dora Siliya amesema wadau hao wana nafasi ya kutoa maoni yao, na wataruhusiwa kutoa maoni yao wakati mswada utakapofikishwa kwenye kamati za bunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako