• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Uganda wakua kwa asilimia 5.8 katika mwaka wa fedha uliopita

    (GMT+08:00) 2018-06-07 10:10:35

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema uchumi wa nchi hiyo uliongeza kwa asilimia 5.8 katika mwaka wa fedha uliopita, na unatarajiwa kuendelea kuongezeka katika mwaka mpya wa fedha.

    Akihutubia taifa, Rais Museveni amesema ongezeko hilo linatokana na ukuaji wa sekta zote za uchumi hasa sekta nne za viwanda (asilimia 6.2), huduma (asilimia 7.3), Tehama (asilimia 7.9) na ujenzi (asilimia 12).

    Pia amesema maendeleo ya kilimo yatasaidia ongezeko zaidi la uchumi wa nchi hiyo. Amesema, serikali itahimiza kilimo cha umwagiliaji na kutoa mbolea kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako