• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwango cha juu cha kujiajiri chatajwa kuwa changamoto ya uhakika wa mapato Afrika kusini mwa Sahara

    (GMT+08:00) 2018-06-07 10:38:14

    Profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Cape Town Bw. Haroon Bhorat amesema kiwango cha juu cha kujiajiri katika eneo la kusini mwa Sahara barani Afrika, kimehatarisha utulivu wa mapato ya familia.

    Akieleza utafiti wake kuhusu ukuaji wa uchumi na kupunguza ukosefu wa usawa katika makao makuu ya Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA nchini Ethiopia, profesa Bhorat amesema sifa muhimu ya soko la ajira barani Afrika ni kuwa karibu asilimia 74 ya watu wanaoweza kufanya kazi katika eneo la kusini mwa Sahara barani Afrika wanajiajiri, badala ya kuajiriwa.

    Kwa mujibu wa profesa Bhorat, asilimia 77 ya watu wanaojiajiri wamejikita katika sekta ya kilimo, jambo ambalo amesema limekuwa changamoto kubwa ya uhakika wa mapato ya familia.

    Ameongeza kuwa ukosefu wa ajira si changamoto kubwa katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara, changamoto kuu katika eneo hilo ndio wafanyakazi maskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako