• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kutokana na mlipuko Baghdad yafikia 14

    (GMT+08:00) 2018-06-07 10:51:02

    Idadi ya vifo kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea jana mashariki mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, imefikia 14, na watu wengine zaidi ya 90 wamejeruhiwa. Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Wizara ya mambo ya ndani ya Iraq, mlipuko huo ulitokea jana jioni baada ya baruti zilizowekwa kwenye ghala moja kulipuka karibu na msikiti wa Washia mjini Sadr, ngome ya imam Moqtada al-Sadr, ambaye chama chake kilipata ushindi kwenye uchaguzi wa wabunge uliofanyika Mei 12. Idara za usalama zimeanza uchunguzi kuhusu mlipuko huo ili kutambua kama ni ajali au shambulizi la kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako