• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chansela wa Ujerumani asema mapambano makali yatatokea kwenye mkutano wa wakuu wa nchi saba

    (GMT+08:00) 2018-06-07 16:38:37

    Chansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel jana kwenye bunge la nchi hiyo amesema, kuna mgongano mkubwa kati ya Ujerumani na Marekani kuhusu baadhi ya makubaliano yanayoshirikisha pande nyingi, hivyo majadiliano makali yatatokea kwenye mkutano wa wakuu wa nchi saba utakaofanyika karibuni nchini Canada.

    Bi. Merkel amesema, Ujerumani itafanya juhudi kudumisha maoni ya pamoja yaliyofikiwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi saba na mkutano wa kundi la nchi 20 iliyofanyika mwaka jana kuhusu biashara na mabadiliko ya hali ya hewa, hasa kudumisha mfumo wa biashara unaoshirikisha pande nyingi na kupinga kujilinda kibiashara.

    Vilevile amesema atafanya majadiliano na rais Donald Trump wa Marekani kuhusu suala la biashara na makubaliano ya nyukilia ya Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako