• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Moyo wa Shanghai" waelekeza SCO kupata maendeleo mapya

    (GMT+08:00) 2018-06-07 16:49:41

    Mkutano wa kilele wa Shirika la ushirikiano wa Shanghai SCO utafanyika kuanzia tarehe 9 hadi 10 Juni mjini Qingdao, China. Tokea shirika hilo lianzishwe mwaka 2001, nchi zote wanachama zinafuata moyo wa Shanghai ulio wa kuaminiana, kunufaishana, kuwa na usawa, kujadiliana, kuheshimiana kuwepo kwa utamaduni chanya, na kutafuta maendeleo ya pamoja, ili kukuza kuaminiana kisiasa, ushirikiano wenye ufanisi, mawasiliano ya utamaduni, na kuzishirikisha India na Pakistan. Na "moyo wa Shanghai" umekuwa msukumo wa nchi wanachama wa SCO wa kupata maendeleo ya pamoja.

    Nchi wanachama wa SCO zinahusisha bara la Ulaya na Asia, ambazo hali zao zinatofautiana kabisa. Kwa kufuata "moyo wa Shanghai", nchi zote wanachama kubwa au ndogo, zinajadiliana kwa pamoja mipango ya maendeleo. Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha utafiti wa Shirika la SCO cha China Bw. Shi Ze anaona kuwa, ni "moyo wa Shanghai" unaojumuisha nguvu ndani ya shirika hilo, na kulielekeza shirika hilo kupata maendeleo mapya. Bw. Shi Ze anasema:

    "Nchi mbalimbali zenye hali zinazotofautiana za mifumo ya jamii, utamaduni, maadili, na kiwango cha maendeleo ya uchumi, zinatafuta ushirikiano wa uchumi wa kikanda, maendeleo ya pamoja na kulinda utulivu na ustawi kwenye kanda hiyo. Kutokana na msingi huo, naona 'moyo wa Shanghai' utaweza kuendelea kulielekeza shirika la SCO kupata maendeleo mapya."

    Katika miongo kadhaa iliyopita, mwelekeo wa maendeleo ya utandawazi wa uchumi duniani si kama tu umeziunganisha nchi mbalimbali, bali pia umeleta changamoto. Mtaalamu wa Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti cha Iran Bw. Mohsen Shariatinia anaona kuwa, "moyo wa Shanghai" umetoa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi mbalimbali kutatua migogoro na kuhimiza ushirikiano. Bw. Mohsen anasema:

    "Naona kuwa "moyo wa Shanghai" ni chombo muhimu kwetu cha kuhimiza kutatua migogoro na kuimarisha ushirikiano. Katika miaka kadhaa ijayo, bara la Ulaya na Asia hususan sehemu ya Mashariki kwenye bara hilo, ina umuhimu mkubwa kwa nchi zinazojitokeza kiuchumi. Nchi zilizoko kwenye sehemu hiyo zina migogoro lakini pia zina maslahi mengi ya pamoja. 'Moyo wa Shanghai' umetoa mfano wa kuigwa kwa nchi tofauti katika kutatua migogoro kwa njia ya amani na kuimarisha ushirikiano."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako