• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushawishi uwekezaji zaidi wa kigeni katika mikoa ya magharibi na ya kati

    (GMT+08:00) 2018-06-07 18:47:33

    Wizara ya Biashara ya China imesema, China itaelekeza uwekezaji zaidi wa kigeni katika maeneo ya magharibi na ya kati nchini humo.

    Msemaji wa wizara hiyo Gao Feng amesema, maeneo ya kati na magharibi yanapaswa kunakili mafanikio ya maeneo ya majaribio ya biashara huria nchini humo, na kwamba kutakuwa na sera nafuu za kodi, ardhi, na mikopo, na miundombinu mipya inayoungana na nchi jirani.

    Gao amesema, licha ya ushindani mkali katika uwekezaji, China ina uwezo wa juu wa kiviwanda, rasilimali watu kubwa, na mazingira yanayoboreshwa ya kibiashara, hivyo itaendelea kuwa eneo maarufu la uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako