• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Bei ya mbolea kupunguzwa

  (GMT+08:00) 2018-06-07 20:21:06

  Wakulima wa kahawa nchini Kenya wanatarajia kupata mbolea ya bei nafuu baada ya serikali kukubali kutenga shilingi bilioni 1 kuboresha kilimo hicho.

  Kamati ya bunge kuhusu bajeti imesema fedha hizo zitatumika kama ruzuku kununua mbolea itakayouzwa bei nafuu itakayowapunguzia gharama wakulima.

  Muungano wa mbolea nchini ulilalamikia kudorora kwa kahawa kufuatia kuongezwa bei ya mbolea nkabla kuomba bunge kujadili swala hilo.

  Fauka ya hayo , zaidi ya wakulima laki 2 wa kahawa walijiondoa kwenye kilimo baada ya kupata hasara.

  Kahawa inaorodheshwa katika nafasi ya nne kwa kuingiza mapato kwa serikali baada ya Utalii, chai na maua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako