• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la bonde la ufa nchini Kenya lawekeza katika kilimo cha kahawa

    (GMT+08:00) 2018-06-07 20:21:52

    Eneo la Rift Valley linaibuka kama kiongozi katika uzalishaji kahawa huku kilimo cha zao hilo kikififia katika eneo la kati mwa Kenya.

    Hii ni kwa sababu wakulima wengi katika eneo la Kati sasa wanawekeza sana katika miradi ya ujenzi wa nyumba za kibiashara badala ya kilimo cha kahawa.

    Wakulima wengi katika eneo la Rift Valley sasa wanakumbatia kilimo cha kahawa kama chanzo cha mapato kando na majani chai, mahindi na ngano kufuatia ongezeko la hitaji la kahawa katika masoko ya ng'ambo.

    Hali hii inachangiwa na kupungua kwa uzalishaji wa kahawa katika mataifa ya kigeni ambayo huzalisha zao hilo kwa wingi.

    Kulingana na ripoti ya Wakfu wa Utafiti kuhusu Kahawa (CRF) , uzalishaji wa kahawa ulipungua katika eneo la Kati katika msimu uliopita kutokana na hali mbaya ya anga.

    Kwa mfano, uzalishaji kahawa katika kaunti ya Nyeri ulipungua kutoka kilo 35,902,046 hadi kilo 21,060, 572 na kupelekea wakulima kupata hasara kubwa.

    Wakulima wanadai kando na hali mbaya ya anga, walipata hasara kwa sababu ya kushuka kwa bei ya zao hilo katika masoko ya humu nchini na kimataifa.

    Eneo la Rift Valley lilizalishwa tani 65,618.50 ya kahawa katika msimu uliopita ikilinganishwa na tani 19,573.38 katika msimu uliotangulia kwa sababu wakulima wengi waliwekeza katika upanzi wa mmea huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako