Rais Xi Jinping wa China amekutana na rais Narsutan Nazarbaev wa Kazakhstan hapa Beijing, ambapo wamekubaliana kuimarisha urafiki wa kijadi kati ya nchi hizo mbili, na kupiga hatua kwa pamoja katika ustawi wa nchi hizo mbili.
Rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Kazakhstan katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na kuimarisha mawasiliano na uratibu katika mambo ya kimataifa na ya kikanda.
Rais Nazarbaev amesema Kazakhstan itashikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na kusaidiana katika mambo ya kimataifa, na kukuza ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta zote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |