• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hata ya Kocha wa Simba haijulikani baada ya kutookeana jana

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:03:10

    Katika hali isiyotarajiwa, kocha mkuu wa Simba, Pierre Lechantre ametoweka nchini Kenya iliko klabu ya Simba, huku ikiwa haijaeleweka mara moja kama kama amerejea jijini Dar es Salaam ama kwao Ufaransa.

    Inasemekana Lechantre amekasirishwa na uswahili ulioonyeshwa na mabosi wa timu hiyo, huku kukiwa na ukosoaji mkubwa usio na msingi wa namna timu ya Simba inavyocheza kwa sasa hadi kufkia fainali za SportsPesa Super Cup. Kocha msaidizi, Masoudi Djuma ndiye anakaimu nafasi hiyo kwa sasa na ndiye aliyekuwepo kwenye benchi wakati Simba ikicheza na Kakamega Homeboys katika nusu fainali ya SportPesa. Viongozi wa Simba wameshindwa kuwa na majibu wa uhakika juu ya hatma ya Lechantrei. Lechantre alijiunga na Simba mapema mwaka huu na kufanikiwa kuipa taji la Ligi Kuu Bara walilokuwa wamelikosa kwa misimu mitano mfululizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako