• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usajili kwenye klabu kubwa za Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:05:13

    Siku chache baada ya kumalizika kwa ligi za Ulaya na zikiwa zimwbaki siku sita kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia, dirisha la usajili liko wazi na wachezaji nyota sasa wanaangalia ni nani atakwenda wapi kuimarisha kikosi gani. Yaya Toure mchezaji ambaye amemlaani Kocha wa Man City kuwa mbaguzi wa rangi, yuko kwenye mazungumzo na klabu ya WestHam ya Uingereza. Toure aliweka wazi kuwa akiondoka City atapenda kubaki Permier League ili akutane na Man City, na kumuonyesha Guardiola yeye ni nani.

    Na klabu bingwa wa kandanda wa Hispania, Ulaya na dunia, Real Madrid inaonekana kumuwinda mwanasoka wa Brazil Neyamar, ambaye ana mkataba na klabu ya PSG. Kumekuwa na tetesi kuwa klabu ya Real Madrid inataka kuwatema Christiano Ronaldo na Gareth Bale, na kumnunua Neymar. Baada ya ushindi wa magoli matatu kwa moja dhidi ya Liverpool mjini Kiev, Ronaldo na Bale walidokeza kuwa wanaweza kuondoka Real Madrid, na hii imeanza kuonyesha wazi kuwa mlango unaweza kuwa wazi wa Neymar kurudi tena nchini Hispania. Hata hivyo mashabiki wa soka wa klabu ya Real Madrid wameonyesha kutaka Ronaldo aendelee kuwa na klabu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako