• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda na DRC zaweka alama kwenye mpaka wao

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:21:13

    Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeweka alama kwenye mpaka wao kati ya eneo la Rubavu la magharibi mwa Rwanda na wilaya ya Goma ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Hafla ya kuweka mpaka imefanyika kwenye mpaka wa pamoja kati ya Rubavu na Goma ili kuadhimisha Siku ya nane ya Mpaka ya Afrika. Waziri wa ulinzi wa Rwanda Bw James Kabarebe na naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Bw Herny Sakanyi wamesaini makubaliano kuhusu ripoti ya kuweka alama za mpaka.

    Bw. Kabarebe amesema nchi hizo mbili zinatarajiwa kuharakisha kazi za kuweka mpaka kwenye ardhi, kwenye Ziwa la Kivu kabla ya mwaka 2022, ambao ni kipindi cha mwisho kilichowekwa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya nchi wanachama kuweka alama za mipaka yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako