• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la waasi wa Sudan Kusini lasema kiongozi wake anapenda kukutana na rais Kiir

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:21:33

    Kundi kuu la waasi la Sudan Kusini SPLA-IO limesema kiongozi wake aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais Bw. Riek Machar anapenda kukutana na mpinzani wake rais Salva Kiir kama ilivyoombwa na viongozi wa kanda hiyo.

    Kundi hilo limetoa taarifa ikisema Bw. Machar anafurahi kukutana na Kiir kutokana na pendekezo la rais Omar Al-Bashir wa Sudan kuhusu kufanya mazungumzo ya ana kwa ana kati ya viongozi hao hasimu mjini Khartoum.

    Kundi hilo limeongeza kuwa ili kutimiza lengo la amani, Bw Riek Machar atafurahi kukutana na rais Salva Kiir katika nchi yoyote ya Shirika la IGAD, ikiwa ni pamoja na Ethiopia, Kenya na Uganda, au katika nchi yoyote nyingine ikiwemo Mauritania.

    Wiki iliyopita IGAD ilipendekeza rais Kiir wa Sudan Kusini afanye mazungumzo na Bw. Machar kabla ya mkutano ujao wa kilele wa Umoja wa Afrika kufanyika mwezi Julai nchini Mauritania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako