• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahamiaji haramu 186 wa Nigeria waondoka Libya kwa hiari

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:52:44

    Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM nchini Libya limesema wahamiaji haramu 171 kutoka Nigeria wamerudi nchini kwao kufuatia mpango wa kurudi nyumbani kwa hiari wa Shirika hilo. Vituo vya mapokezi ya wahamiaji nchini Libya vimefurika wahamiaji haramu na mamlaka za nchi hiyo zimetoa mwito kwa mashirika ya kimataifa kutoa msaada zaidi kuboresha mazingira ya kimaisha ya vituo hivyo. Mpango wa kurudi nyumbani kwa hiari wa IOM unatoa fursa kwa wahamiaji waishio maisha magumu nchini Libya kurudi nyumbani kwao, na mwaka jana mpango huo uliwasaidia wahamiaji haramu elfu 20 nchini humo kurudi nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako