• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa Brexit unaendelea kukumbwa na vikwazo

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:54:10

    Hofu kuwa waziri wa Uingereza anayeshughulikia mambo ya nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya Bw David Davis atajiuzulu kutokana na tofauti kati yake na waziri mkuu Bibi Theresa May, imeondoka baada ya wawili hao kufanya mazungumzo jana.

    Tofauti kati ya mawaziri hao ilionekana kuwa kikwazo katika mchakato wa Brexit. Hata hivyo baada ya tofauti zao kuondolewa, vyombo vya habari vimemnukuu waziri wa nchi katika ofisi ya wizara inayoshughulikia mambo ya nje na ya jumuiya ya madola, Bw. Alan Duncan akisema kutokana na tofauti zilizopo kuhusu masharti ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, kuna uwezekano wa kuwepo kwa upigaji kura za maoni wa pili kuhusu makubaliano ya masharti ya kujitoa Umoja wa Ulaya, lakini amesema haiwezekani kuwa na kura za pili za maoni kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya au la.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako