• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya asikitishwa na vifo vya watu kwenye ajali ya ndege

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:55:04

    Abiria wote na wafanyakazi wa ndege ya Fly-SAX ya Kenya wamefariki kutokana na ajali ya ndege hiyo iliyoanguka katika mlima wa Aberdare.

    Rais Uhuru Kenyatta amesema anasikitishwa na ajali hiyo, na kuahidi kuwa serikali ya Kenya itatoa misaada yote kwa wafiwa. Pia amesema, watachunguza kikamilifu chanzo cha ajali hiyo.

    Rais Kenyatta alitoa kauli hizo baada ya kikosi cha uokoaji kugundua miili ya watu hao 10, mabaki ya ndege, na kisanduku cheusi kwenye msitu wa Aberdare.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako