• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpira wa Kombe la dunia kuwafurahisha magolikipa

  (GMT+08:00) 2018-06-08 10:04:18

  Wanasayansi wa mwendo wamesema mpira mpya uliotengenezwa na kampuni ya Adidas kwa ajili ya fainali za kombe la dunia, ni mpira imara-- pengine ni imara hata kuliko Jabulani, uliotumika kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 ambao ulikosolewa sana. Baadhi ya magolikipa wamesema mpira huo ni mgumu kuunyaka, na unaweza kusababisha mvua za magoli kama magolkipa hawatakuwa makini. Telstar 18 unafanana na mpira wa kwanza wa Adidas wa fainali za Kombe la Dunia ulioitwa Telstar, ambao ulitumiwa nchini Mexico mwaka 1970. Wanasayansi wamesema watakuwa wakifuatilia kila hatua ya mchezaji na mwenendo wa mpira, wakichunguza kila nyanja, kwa kuzingatia masuala kama ya jinsi unavyotembea hewani, saikolojia na mwili wa binadamu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako