Biashara ya nje ya China imeongezeka kwa asilimia 8.8 katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho, na kufikia dola za kimarekani trilioni 1.82.
Takwimu zilizotolewa na Idara ya Forodha ya China zimeonyesha kuwa, uuzaji wa bidhaa kwa nje nchini China uliongezeka kwa asilimia 5.5 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Mei mwaka huu, huku uagizaji wa bidhaa ukiongezeka kwa asilimia 12.6.
Idara hiyo imesema, katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu, uagizaji na uuzaji wa bidhaa chini ya kipengele cha biashara iliongezeka kwa asilimia 12.7 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |