• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar latoa mchango kwa mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za jumuiya ya SCO

    (GMT+08:00) 2018-06-08 17:11:48

    Kutokana na kuungwa mkono na sera nafuu za taifa, eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar mkoani Xinjiang limekuwa moja ya maeneo muhimu ya maendeleo ya uchumi na biashara yanalovutia uwekezaji, teknolojia na watu wenye ujuzi wa ndani na nje ya nchi. Eneo hilo limeonesha umuhimu mkubwa katika kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO.

    Kanda ya Kashgar ina bandari 5 kavu za ngazi ya kwanza ya taifa, zinazowasiliana na nchi 8 za Kyrgyzstan, Tajikistan, Afghanistan, Pakistan, India, Uzbekistan, Turkmenistan na Kazakhstan. Sehemu kubwa ya nchi hizo ni wanachama au nchi wachunguzi wa Jumuiya ya SCO. Tangu lilipoanzishwa rasmi mwaka 2010, eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar limepata maendeleo makubwa. Mkurugenzi wa eneo la ulinzi wa ushuru la eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar Bw. Bai Can amesema,

    "Kashgar ina ubora wa kuwa mahali maalumu, miji yote muhimu ya kiuchumi ya nchi za Asia Kusini na Asia Kati za Ukanda Mmoja na Njia Moja na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya SCO ziko ndani ya umbali wa safari ya ndege kwa saa moja na nusu kutoka Kashgar. Hivyo Kashgar ni mji muhimu sana kwenye mkakati wa kitaifa kuhusu kufungua mlango kwa nchi za Magharibi mwa China. "

    Kwenye kiwanda cha nguo cha Meili'ao cha Xinjiang, wafanyakazi wanatengeneza nguo zitakazouzwa Asia ya Kati. Kiwanda hicho ni kiwanda cha Shenzhen kinachosaidia mkoa wa Xinjiang. Baada ya kuanzishwa kwenye eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar, nguo za kiwanda hicho zinasafirishwa kwenda Asia Kati na Asia Kusini kwa siku 45, lakini hivi sasa nguo zake zinasafirishwa kwa Asia Kati na Asia Kusini kutoka Kashgar kwa siku 15.

    Hivi sasa kampuni nyingi zaidi zimeanza kuingia kwenye eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar, na kufanya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nchi za Jumuiya ya SCO. Mkurugenzi wa kampuni ya nguo ya Jinfujie ya Xinjiang Bw. Wei Jianyong amesema, hivi karibuni kampuni yake imesaini makubaliano ya ushirikiano na kampuni za Pakistan na Tajikistan. Anasema,

    "Tunapanga kutengeneza nguo za chapa tatu za Tajikistan, tutaendelea na mazungumzo na upande wa Tajikistan mwezi Julai. Idadi ya nguo hizo inakadiriwa kufikia laki 37, na thamani ya biashara ya orodha hiyo ya kuagiza inakadiriwa kufikia yuan milioni 76."

    Katika siku za baadaye, eneo la kujiendeleza kiuchumi la Kashgar litafanya juhudi kuhimiza usafirishaji kwa njia ya barabara ya kimataifa kati ya China na Kyrgyzstan na Uzbekistan, na barabara kati ya China na Pakistan, ili kuhimiza zaidi mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya SCO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako