• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China akutana na rais wa Russia

  (GMT+08:00) 2018-06-08 18:55:00

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amekutana na rais Vladimir Putin wa Russia ambaye yuko ziarani China ambapo pia atahudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO utakaofanyika mjini Qingdao.

  Bw. Li amesema, China inapenda kuimarisha kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na Muungano wa kiuchumi wa Ulaya na Asia, kuendelea kupanua biashara kati ya pande mbili na kuhimiza miradi ya ushirikiano ya nishati ya mafuta na gesi asili. Pia kujadili kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, anga ya juu na fedha, na kuinua uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati na kiwenzi wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

  Rais Putin amesema, Russia inapenda kuunganisha mikakati ya maendeleo na China, kusukuma mbele ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali, kuzidisha mawasiliano ya utamaduni, na kuhimiza uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kupata mafanikio zaidi chini ya uratibu wa SCO na mifumo mingine ya pande nyingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako