• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ruwaza ya 2030 yalenga kufanya vijana wabuni kazi za kujitegemea

  (GMT+08:00) 2018-06-08 20:19:14

  Mkurugenzi wa Mipango na Programu katika Wizara ya Ugatuzi na Mipango nchini Kenya Bw Isaac Kamande amesema serikali inatilia maanani ruwaza ya 2030 kwa lengo la kuwapa mwongozo vijana wabuni kazi za kujitegemea bila kusubiri kuajiriwa. Amesema serikali inatilia mkazo masomo ya kiufundi kwa lengo la kuwapa vijana nafasi ya kujitegemea katika siku za usoni. Ameongeza kuwa lengo kuu kwa sasa ni kuona ya kwamba kila sekta serikalini inalenga ajenda nne muhimu za serikali ambazo ni makazi, ujenzi wa viwanda, maswala ya afya na uhifadhi wa chakula. Bw Kamande amesema hiyo ndiyo ajenda muhimu ya Rais kwa muda wa miaka minne ijayo.Alikadiria ya kwamba itakapofika mwaka wa 2030 idadi ya Wakenya itafika takribani 60 milioni huku akisema ni vyema kuwa na mipangilio maalumu ya kuendeleza maisha ya idadi hiyo ya watu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako