• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msako dhidi ya mashine za biashara ya kamari waendelea

    (GMT+08:00) 2018-06-08 20:19:33

    Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya Bw. Fred Matiang'i amesema hatalegeza msimamo wake na jitihada zake kumaliza michezo haramu ya kamari nchini Kenya. Matiang'i amewataka vigogo wa usalama na washirikishi wa maeneo katika kaunti zote kujitahidi kuondoa mashine hizo. Amesema mashine za biashara hiyo zinaingizwa Kenya kinyume na sheria na kwamba zimechangia pakubwa kupotosha nidhamu ya vijana. Ameeleza kushangazwa kwake na athari za mashine hizo kusababisha baadhi ya watoto kugura masomo ili kucheza kamari.Ameongeza kuwa msako wa bidhaa ghushi unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini Kenya unajumuisha mashine hizo. Waziri huyo alisema uwekezaji wa mashine hizo hauna manufaa yoyote kwa taifa, ila vijana kupoteza mapato yao kwa kamari. Operesheni ya kuondoa mashine za kamari nchini ilianza mwaka uliopita, 2017, kupitia agizo la waziri huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako