• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping akutana na baadhi ya viongozi walioko China kuhudhuria mkutano wa SCO

    (GMT+08:00) 2018-06-09 19:05:27

    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na baadhi ya viongozi walioko China kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai SCO.

    Rais Xi alipokutana na mwenzake wa Pakistan Mamnoon Hussain amesema, China inatilia maanani sana uhusiano kati yake na Pakistan, inapenda kushirikiana na nchi hiyo kusukuma mbele ushirikiano wa pande mbalimbali zikiwemo nishati, miundo mbinu, na ugaidi, na kuhimiza uhusiano huo kuendelea zaidi.

    Naye rais Hussain amesema China ni rafiki wa dhati na mwenzi imara wa Pakistan, na uhusiano kati ya Pakistan na China haubadiliki.

    Alipokutana na rais Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan, rais Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Uzbekistan umeendelea kwa kina, China inapenda kutimiza ustawi wa pamoja na Uzbekistan.

    Rais Mirziyoyev amesema nchi yake inapenda kuongeza ushirikiano halisi na China kwa mujibu wa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kuzidisha mawasiliano na uratibu na China katika mambo ya kikanda.

    Rais Xi leo pia amekutana na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi, na rais Emomali Rakhmonov wa Tajikistan.

    Mkutano wa 18 wa kamati ya viongozi wa nchi wanachama wa SCO utafanyika kesho mjini Qingdao, China. Hadi kufikia leo alasiri, viongozi wote wa nchi wanachama na waangalizi wa jumuiya hiyo wamefika mjini Qingdao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako