• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto milioni 1.25 nchini Somalia kupata utapiamlo kwa sababu ya mafuriko

    (GMT+08:00) 2018-06-09 19:14:58

    Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF, jana limesema kwa mwaka huu zaidi ya watoto million 1.25 wanatarajiwa kuwa na utapiamlo nchini Somalia kutokana na mafuriko.

    Taarifa ya ripoti hiyo ya UNICEF imetolewa na Msemaji wa UN Stephan Dujarric katika mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya UN ambapo alisema mafuriko yaliyoanza tangu mwezi April ndio yamesababisha.

    Akisema kuwa, nusu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano au zaidi ya milioni 1.25 wataugua utapiamlo, wakiwemo watoto 232,000 ambao wataathirka zaidi na utapiamlo na watahitaji uangalizi maalum wa kiafya ili kuokoa maisha yao.

    Dujarric amesema katika maeneo mengi yaliyoathirika kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa surua na kipindu pindu ambacho ni tishio zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako