• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping aongoza mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai

  (GMT+08:00) 2018-06-10 09:30:29

  Mkutano wa 18 wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai umefunguliwa leo asubuhi huko Qingdao, mashariki mwa China.

  Rais Xi Jinping wa China, ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo, ameongoza mkutano wa wakuu wa nchi nane wanachama, ambazo ni China, Russia, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Uzbekistan, India na Pakistan.

  Huu ni mkutano wa kwanza wa kilele tangu jumuiya hiyo ikubali uanachama wa India na Pakistan mwaka jana. Habari zinasema, viongozi hao watabadilishana maoni kuhusu hali ya jumuiya hiyo, ushirikiano kati ya nchi wanachama na masuala muhimu ya kikanda na kimataifa. Pia watasaini Azimio la Qingdao pamoja na nyaraka zaidi ya 10 zinazohusu ushirikiano katika nyanja za usalama, uchumi na utamaduni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako