• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China asema SCO imevumbua njia mpya ya ushirikiano wa kikanda

  (GMT+08:00) 2018-06-10 11:38:20

  Rais Xi Jinping wa China ameeleza kufurahia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai tangu ianzishwe miaka 17 iliyopita, na kufafanua kwamba nchi wanachama tayari zimejenga uhusiano wa kiwenzi wenye sifa za kutofungamana, kutopingana wala kutolenga upande wa tatu.

  Rais Xi ameusifu uvumbuzi muhimu kwa nadharia za uhusiano wa kimataifa na utekelezaji wake, kwamba jumuiya hiyo imevumbua njia mpya ya ushirikiano wa kikanda na kutoa mchango kwa amani na maendeleo ya kanda yake.

  Rais Xi pia amesisitiza kuwa, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai yenye asilimia 20 ya nguvu ya uchumi wa dunia na asilimia 40 ya idadi ya watu duniani, imekuwa nguvu muhimu katika kuhimiza amani na maendeleo na kulinda haki duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako