• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping asisitiza kupinga hatua yoyote ya kujilinda kibiashara

  (GMT+08:00) 2018-06-10 14:38:04

  Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kupinga hatua yoyote ya kujilinda kibiashara.

  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO, rais Xi Jinping amesema, utandawazi wa kiuchumi na umoja wa kikanda ni mkondo wa enzi ya sasa. Amesema pande zilizoshiriki mkutano huo zimejizatiti kutetea heshima na ufanisi wa kanuni za Jumuiya ya biashara ya kimataifa, na kuimarisha mfumo wa biashara wa pande zote. Ameongeza kuwa pande hizo zitaendelea kushikilia kanuni ya kunufaishana, kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, pamoja na kuunganisha mikakati ya maendeleo ya pande mbalimbali. Pia rais Xi amesema pande hizo zitazidi kushirikiana katika nyanja za uchumi na biashara, uwekezaji, mambo ya fedha, ujenzi wa mawasiliano na kilimo, kurahisisha biashara na uwekezaji, na kufanikisha maendeleo ya pamoja katika kanda hiyo, ili kuwanufaisha watu wa nchi mbalimbali za kanda hiyo na kuwa injini ya ongezeko la uchumi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako