• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia 90 wapatiwa chanjo ya Ebola nchini DRC

    (GMT+08:00) 2018-06-10 19:04:05

    Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Oly Ilunga amesema tangu kuanzishwa oparesheni katika jimbo Ikweta takribani asilimia 90 ya wagonjwa walioripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola wamepatiwa chanjo za kiafya.

    Ilunga amewaambia waandishi wa habari kuwa chanjo na matibabu ya bure, pamoja na elimu kwa umma kwenye kanda za kiafya za eneo la Bikoro zilizoathirika na ugonjwa huo, vimeleta matokeo chanya katika kukabiliana na virus vya ugonjwa wa Ebola katika jimbo la Ikweta.

    Tangu kugundulika kwa ugonjwa huo mwezi Mei, vipimo vya maabara vilithibitisha kuwa takribani wagonjwa 38 kuambukizwa katika kanda ya kiafya ya Bikoro, kukiwa na vifo 27 na 13 wakithibitika kuwa ni kutokana na Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako