• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri na Ethiopia zakubaliana juu ya mtazamo mpya juu ya ujenzi wa bwawa nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-06-10 19:15:34

    Msemaji wa rais wa Misri, Bassam Rady amesema Misri na Ethiopia zimekubaliana kuwa na mtazamo wa pamoja kuhusu mradi wa ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme nchini Ethiopia GERD.

    Mtazamo huo uliofikiwa baina ya rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali, uko katika msingi wa kila upande kuheshimu haki za kimaendeleo na maslahi ya upande mwingine.

    Waziri wa Ethiopia aliwasili mjini Cairo nchini Misri jana kwa ajili ya ziara, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu achukue wadhifa huo mwezi April mwaka huu.

    Katika mkutano wao, viongozi wawili hao walionyesha nia ya kusukuma mbele uhusiano na ushirikiano wa nchi zao mbili kwenye sekta zote, hasa kisiasa na kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako