• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano mkuu wa G7 wafungwa

    (GMT+08:00) 2018-06-10 19:30:02

    Mkutano mkuu wa mwaka wa kundi la nchi 7, G7 umefungwa jana, ambapo rais Donald Trump wa Marekani alitoa kauli kali kuhusu suala la biashara, na akisema mgogoro kati ya nchi hizo 7 umezidi kuwa mbaya. .

    Baada ya mkutano huo nchi hizo 7 zilitoa taarifa ya pamoja kuhusu kunufaika na ongezeko la uchumi kwa haki na usawa, usawa wa kijinsia, na kuwakabidhi wanawake haki, amani na usalama wa dunia, fursa za ajira za siku za baadaye, mabadiliko ya hali ya hewa na bahari.

    Jana asubuhi rais Trump aliyetangulia kuondoka kwa ajili ya kwenda Singapore, kabla ya kuondoka, alisema alifanya mazungumzo na viongozi wa nchi nyingine na kujadili umuhimu wa biashara yenye usawa na kunufaishana na njia ya kukabiliana na suala la Iran. Alisisitiza kuondoa ushuru, vikwazo vya biashara au misaada ya fedha, na pia akisisitiza kuwa Marekani itachukua hatua zote ili kuzuia vitendo visivyokuwa na usawa vya kibiashara. Lakini Rais Trump alisema kwenye vyombo vya habari kuwa kutokana na maelezo ya hatua zitakazochukuliwa na Canada yaliyotolewa na waziri mkuu wa Canada ya kukusanya ushuru mwingi kwa wakulima, wafanyakazi na makampuni ya Marekani kwa Canada, amewaambia wajumbe wa Marekani kutounga mkono taarifa ya pamoja ya kundi la nchi 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako