• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na baadhi ya viongozi wa SCO

    (GMT+08:00) 2018-06-10 19:51:07

    Rais Xi Jinping wa China leo mjini Qingdao, kwa nyakati tofauti amekutana na baadhi ya viongozi waliopo China kwa ajili ya mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai.

    Rais Xi alipokutana na rais Ashraf Ghani wa Afghanistan amesema China na Afghanistan ni majirani wema, na siku zote zinaungana mkono, kuaminiana na kusaidiana. Kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili ni msimamo usiobadiliki wa serikali ya China. rais Xi pia amesisitiza kuwa kifunguo cha Afghanistan kutimiza amani na usalama wa kudumu ni mchakato wa maafikiano wa kisiasa unaoongozwa na waafghanistan.

    Rais Ghani amesema nchi yake inaishukuru China kwa kutoa misaada katika muda mrefu uliopita, na uungaji mkono kwa mchakato wa amani nchini Afghanistan.

    rais Xi leo pia amekutana na rais Alexandr Lukashenko wa   Belarus.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako