• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 40 wauawa kwenye mapambano kati ya jeshi la Yemen na kundi la Houthi

    (GMT+08:00) 2018-06-11 08:50:10

    Watu 40 wameuawa na wengine makumi wamejeruhiwa kwenye mapambano makali yaliyoibuka jana kati ya jeshi la Yemen na kundi la waasi wa Houthi mkoani Al Ḥudaida, magharibi mwa Yemen. Kwa mujibu wa Chanzo cha habari kutoka idara ya afya ya mkoa huo, katika saa 24 zilizopita, jeshi la serikali na kundi la Houthi wamepambana vikali kwenye maeneo mengi mkoani humo na kusababisha vifo vya wanajeshi saba wa jeshi la serikali na waasi 33 wa Houthi. Katika wiki zilizopita, muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeanzisha operesheni za kutwaa mji wa Ḥudaida, licha ya Umoja wa mataifa kutoa onyo kuwa operesheni hizo zitazusha janga la kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako