• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchi Ethiopia akanusha upotoshaji kuhusu ushiriki wa China nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-06-11 09:11:11

    Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Tian Jian, amesema upotoshaji unaoenezwa kuhusu uwepo wa shughuli za China nchini Ethiopia hauendani na hali halisi.

    Bw. Tian jian amesema hayo kufuatia habari za upotoshaji kuhusu ushirikiano kati ya China na Ethiopia, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa uwekezaji wa China nchini Ethiopia, kuwa ripoti hizo sio za kweli.

    Bw. Tian amekumbusha kuwa uwekezaji wa moja kwa moja toka China kwenda Ethiopia tangu ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili uanzishwe, umeongezeka mara mbili kati ya mwaka 2015 na 2017.

    Bw. Tian pia amekanusha upotoshaji kuhusu pendekezo la "ukanda mmoja, njia moja" kuwa linapeleka viwanda vilivyopitwa na wakati na uchafuzi.

    Bw. Tian ametolea mfano wa kiwanda cha dawa cha Sansheng na viwanda vingine vya China nchini Ethiopia, na kusema viwango vya teknolojia vya viwanda hivyo vinafanana na vya nchi zilizoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako