• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yawafikisha mahakamani watu 28 kutokana na kuanzisha kampeni ya kuipinga serikali

    (GMT+08:00) 2018-06-11 09:11:33

    Idara kuu ya mwendesha mashtaka ya Misri imewafungulia mashtaka ya jinai watu 28, ikiwa ni pamoja na watu 19 wanaotafutwa na 9 walio gerezani, kutokana na kuchochea migomo, na kuvuruga amani na umoja wa kitaifa.

    Taarifa iliyotolewa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali, inasema watu hao pia wanatuhumiwa kuanzisha kundi haramu linaloitwa "baraza la mabadiliko la Misri" lenye lengo la kupinga taasisi za serikali. Taarifa imeongeza kuwa kundi hilo linatoa fedha kuhimiza mabavu, kuchochea migomo na kueneza habari za upotoshaji ndani na nje ya Misri.

    Tangu utawala wa Rais Mohamed Morsi wa Misri uondolewe madarakani mwaka 2013, Misri imekuwa inapambana na mawimbi ya mashambulizi ya kigaidi, yaliyosababisha vifo vya mamia ya polisi na wanajeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako