• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria afanya ziara Morocco

    (GMT+08:00) 2018-06-11 09:26:09

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria yuko nchini Morocco kwa ziara ya siku mbili nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na serikali ya Morocco, inasema wakati wa ziara yake, Rais Buhari anatarajiwa kufanya mazungumzo na mfalme Mohammed wa sita na kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano mbalimbali.

    Katika miaka kadhaa iliyopita, uhusiano kati ya Nigeria na Morocco umekuwa na maendeleo makubwa. Wakati wa ziara ya mfalme wa Morocco nchini Nigeria mwezi Desemba mwaka 2016, nchi hizo mbili zilisaini makubaliano kadhaa, na pia kuhitimisha ushirikiano muhimu kuhusu bomba la gesi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako