• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Azimio la Qingdao latoa wito wa mwafaka wa pamoja kukabiliana na changamoto za kimataifa

  (GMT+08:00) 2018-06-11 09:45:08

  Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO wametoa azimio katika mkutano wa kilele wa mwaka uliofanyika jana mjini Qingdao, China, wakitoa mwitio kwa jumuiya ya kimataifa kutafuta mwafaka wa pamoja na kukabiliana kwa ufanisi na changamoto za kimataifa.

  Mkutano wa 18 wa baraza la viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo umetoa wito huo, wakati siasa za kimataifa zenye ncha nyingi zikizidi kujitokeza na hali zisizotabirika zikizidi kuongezeka. Nchi wanachama wa jumuiya hiyo zimetoa dhana ya pamoja "Kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja."

  Azimio hilo pia limesema, ushiriki wa India na Pakistan kwenye jumuiya ya SCO umeinua ushirikiano katika sekta mbalimbali hadi kwenye ngazi mpya.

  Habari nyingine zinasema, rais Xi Jinping wa China huko Qingdao amekutana na mwenzake wa Mongolia Khaltmaagiin Battulga. Rais Xi amesema, Mongolia ikiwa ni nchi ya uangalizi ya kwanza ya jumuiya ya SCO, China inaiunga mkono Mongolia kuinua kiwango cha ushirikiano wa jumuiya hiyo, na kwamba China inapenda kushirikiana na Mongolia, Russia katika kutekeleza mwongozo wa mpango wa njia ya kiuchumi kati ya nchi hizo tatu na kuhimiza ushirikiano kati ya pande tatu kupata maendeleo mengi zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako