• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia, Bado siku 3: Mahojiano na Rais wa FIFA

    (GMT+08:00) 2018-06-11 10:00:38

    Rais wa Shirikisho wa Vyama vya soka duniani FIFA, Gianni Ifantino amekamilisha zoezi lake la kukagua na kupokea ripoti za ukamilifu maandalizi ya michuano.

    Baada ya kukamilisha, Infantino alifanya mahojiano maalum mwishoni mwa wiki hii, ambapo alizungumzia masuala makuu matatu kama ifuatavyo;

    Kwa alianza kwa kuthibitisha kuwa kamati ya maandalizi ya kitaifa kwa ajili ya michuano hiyo na serikali kwa ujumla wamekamilisha kwa asilimia 100 hatua zote za msingi, hivyo taifa la Urusi liko tayari kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika kwa mwezi mmoja, viwanja vipo tayari, makazi na malazi, miundo mbinu ya usafiri.

    Akisema FIFA kwa upande wao wamekamilisha pia sehemu muhimu zinazowahusu moja kwa moja ikiwemo uratibu wa timu shiriki, sheria pamoja na waamuzi.

    Suala la pili alilozungumzia ni usalama wakati wa michuano hiyo, dhidi ya vitendo vya kihalifu na vitendo vya ubaguzi, akisema FIFA tayari ina kanuni zinazoongoza mambo hayo na kwamba zitafuatwa ikiwemo adhabu inapobidi endapo kutatokea ukiukwaji.

    Lakini zaidi akisema sekta ya usalama ya Urusi tayari imeimaimarisha usalama kwa kushirikiana na idara zingine za usalama za kimataifa na imejipanga ili kuhakikisha msimu huu wa kombe la dunia unafanyika katika mazingira salama.

    Lakini mwisho wa yote, Bwana Infantino alitoa rai kwa wote wanaosafiri kwenda Urusi kufurahia mashindano haya, kwamba watakaribishwa kwa wema na wanahakikishiwa usalama kwa asilimia 100, lakini kwa wale ambao wanafikiria kwenda kuleta shida ni bora wakabaki huko huko majumbani kwao kwa sababu wao ndio watapata shida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako