• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia 2018, Bado siku 3: Maoni ya Mchezaji wa zamani

    (GMT+08:00) 2018-06-11 10:00:56

    Kwingineko mchezaji aliyewahi kutamba na kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, na aliyefanikiwa kuwemo katika kikosi cha dhahabu, kilichotwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2010, kilichoshiriki miichuano ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 na mwaka 2012. Xabi Alonso alipoulizwa kuhusu maoni yake, kuhusu timu shiriki za michuano ya kombe la dunia mwaka huu amesema, ni Hispania.

    Alonso ambaye jana amemaliza masomo ya mwaka ukufunzi wa soka (ukocha) amesema kikosi cha kocha wa sasa Julien Lepetegui, kimesheni vipaji vilivyoanza kutengenezwa miaka kadhaa iliyopita na vikaendelezwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo kucheza katika ligi kubwa na bora duniani zenye ushindani mkubwa akiwatolea mfano, Diego Costa, Marco Asensio na Jodi Alba.

    Akiwa na timu hiyo ya Hispania, Alonso amecheza mechi 114 tangu ajiunge nayo mwaka 2003 hadi alipostaafu mwaka 2014 baada ya kombe la dunia nchini Brazil.

    Kwa upande wa klabu, ametumikia vilabu vikubwa vya ulaya kwa nyakati tofauti na kwa mafanikio makubwa Liverpool (2004-09), Real Madrid (2009-14) na Bayern Munich 2014-17).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako