• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, SportPesa Super Cup: Gor Mahia watetea ubingwa

  (GMT+08:00) 2018-06-11 10:22:46

  Gor Mahia wamefanikiwa kutetea taji la michuano ya Sportpesa Super Cup baada ya kushinda kwa magoli 2-0 kwenye mechi ya fainali jana dhidi ya Simba mjini Nakuru.

  Magoli ya Gor yalifungwa na washambuliaji wawili wa kimataifa kutoka Rwanda Meddie Kagere na Jacques Tuyisenge.

  Kwa ushindi huo, Gor sasa wamejipatia kombe, medali, pesa shilingi za Kenya milioni 3 na nafasi ya kwenda Uingereza kucheza mechi ya Kirafiki na Everton inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza ambapo itakuwa ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana kwani mwaka jana pia zilicheza.

  Katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu, Singida United ya Tanzania iliifunga timu ya Kakamega Homeboys kwa penati 4-1 baada ya dakika 90 za kawaida za mechi ya hiyo kuisha kwa sare ya magoli 1-1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako