• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaanza wiki ya kueneza kubana matumizi ya nishati

    (GMT+08:00) 2018-06-11 18:19:45

    Wiki ya 28 ya kueneza kubana matumizi ya nishati imeanza rasmi leo, na kauli mbiu ya mwaka huu ni "kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi anga ya kibuluu". Maofisa wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China na wizara ya uhifadhi wa mazingira ya China wameeleza kuwa, katika miaka mitano iliyopita, kiwango cha matumizi ya nishati katika uzalishaji mali kimepungua kwa asilimia 20, na kasi ya ongezeko la utoaji wa Carbon Dioxide imepungua.

    Kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo, naibu mkurugenzi wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Ning Jizhe amesema, matumizi ya nishati ya uzalishaji mali nchini China kati ya mwaka 2013 hadi 2017 yamepungua kwa asilimia 20.9, ambayo ni sawa na kupunguza matumizi ya makaa ya mawe zaidi ya bilioni moja. Anasema,

    "China itatekeleza kwa makini utaratibu wa kudhibiti kiasi na kasi ya matumizi ya nishati, kuboresha muundo wa nishati zinazotumika, na kuongeza kutumia nishati safi badala ya makaa ya mawe. Vilevile China itaendeleza sekta za uhifadhi wa mazingira, uzalishaji mali usiosababisha uchafuzi, na nishati safi, pia itaeneza kwa nguvu bidhaa, teknolojia, vifaa na huduma za kubana matumizi ya nishati."

    Hivi sasa namna ya kupunguza utoaji wa Carbon Dioxide ni moja ya masuala muhimu ya uhifadhi wa mazingira. Katika wiki ya mwaka huu ya kueneza ufahamu wa kubana matumizi ya nishati, China itafanya shughuli za siku ya kupunguza utoaji wa Carbon Dioxide, ili kuwafahamisha zaidi wananchi kuhusu changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa. Naibu waziri wa uhifadhi wa mazingira ya China Bw. Zhuang Guotai anasema,

    "Mwaka jana kasi ya ongezeko la utoaji wa hewa ta Carbon Dioxide nchini China ilipungua kwa asilimia 46. Hatua yetu ijayo ina lengo la kuonesha vya kutosha mchango muhimu wa kupunguza utoaji wa Carbon Dioxide kwa maendeleo endelevu ya uchumi na jamii, kuweka uwiano wa viumbe, uhifadhi wa mazingira, na kuhimiza juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa."

    Shughuli mbalimbali za kuhimiza vitendo vya kuhifadhi mazingira pia zimefanyika leo, kama vile kulipa pesa ya maegesho ya gari bila kusimamisha gari, kurekebisha matumizi ya kiyoyozi, na kuchunguza matumizi ya nishati ya mashirika yanayotumia nishati zaidi. Naibu meya wa Beijing Bw. Yang Bing anasema,

    "Tunatumai kila mtu atashiriki kwenye juhudi za kuhifadhi mazingira, kwa mfano kupunguza matumizi ya magari, kutumia mashine zenye matumizi madogo ya umeme majumbani, kutumia viyoyozi kwa njia inayofaa zaidi, na kuzingatia uhifadhi wa mazingira."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako