• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mgogoro wa ushuru kati ya Marekani, Canada na nchi za Ulaya wazidi kuwa mbaya

  (GMT+08:00) 2018-06-11 18:37:06

  Canada na nchi za Ulaya zimeilaani Marekani kuhusu suala la ushuru na taarifa za uongo kuhusu Canada baada ya mkutano mkuu wa kundi la nchi 7 uliofanyika huko Quebec.

  Waziri mkuu wa Canada Bw. Justin Trudeau jana alitangaza kuwa nchi zote wanachama wa kundi hilo zilisaini taarifa ya pamoja, lakini alibainisha kuwa suala la ushuru wa Marekani ni fedheha na Canada haitakubali kuamrishwa.

  Kauli hiyo imemuudhi rais Donald Trump wa Marekani na kuwaamrisha wasaidizi wake kutosaini taarifa ya pamoja ya kundi la nchi 7 kwa madai ya taarifa za uongo zilizotolewa na Bw. Trudeau, na kutokana na ukweli kuwa Canada inatoza ushuru mkubwa kwa wakulima, wafanyakazi na makampuni ya Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako