• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuhimiza ushirikiano wa SCO kuwa na ufanisi zaidi

  (GMT+08:00) 2018-06-11 19:15:27

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China itashirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai SCO kutekeleza kwa pande zote matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Qingdao. ,

  Bw. Geng Shuang pia amesema China itahimiza SCO iwe mshikamano zaidi, ushirikiano wenye ufanisi zaidi, utendaji wenye nguvu zaidi, na mustakabali mzuri zaidi. Pia amesema mkutano huo wa Qingdao umeweka mambo mapya kwenye "moyo wa Shanghai", kuthibitisha lengo jipya la SCO, na kuweka mwongozo mpya wa utekelezaji wa ushirikiano katika siku za usoni.

  Kuhusu mkutano wa G7, Bw. Geng Shuang amesema, China siku zote inatetea nchi mbalimbali kuendeleza uhusiano juu ya msingi wa kuheshimiana, kutendeana kwa usawa, na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine. Pia China inatetea nchi mbalimbali kufanya ushirikiano wa pande nyingi kwa wazi, shirikishi na kutolengea pande ya tatu, na kufuata mkondo wa zama hizi wa maendeleo ya amani na ushirikiano wa kunufaishana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako