• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Mfumuko  wa bei unaenda chini kutokana na kupanda kwa bei ya chakula

  (GMT+08:00) 2018-06-11 20:29:57
  Mfumuko wa bei wa kila mwaka wa mwezi Mei, 2018 ulipungua kwa asilimia 3.6 ikilinganishwa na mwezi uliopita, kutokana na mabadiliko kidogo ya bei ya chakula.

  Mkurugenzi, wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) bw Ephraim Kwesigabo aliiambia waandishi wa habari kuwa kiwango cha mfumuko wa bei kwa mwezi ulipungua hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.8 iliyoandikwa mwezi Aprili.

  Mkurugenzi amesema kushuka kwa mfumuko wa bei kumetokana na kushuka kwa bei ya bidhaa za chakula.

  Aidha amesema nchi zengine za Mashariki mwa Afrika, kama vile Uganda hali ya mfumuko wa bei ya mwezi Mei 2018 ilipungua hadi asilimia 1.7 kutoka asilimia 1.8 iliyoandikwa mwezi wa Aprili 2018 na nchini Kenya mwezi Mei 2018 mfumuko wa bei uliongezeka na kufikia asilimia 3.95 kutoka asilimia 3.73 iliyorekodiwa mwezi wa Aprili 2018

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako