Munya amezitaka serikali za kaunti kuacha kutoza ushuru mara mbili kwa malori yaliyo kwenye safari, ni kinyume na katiba .
Munya alikuwa akizungumza Kitale wakati wa warsha ya kuhamasisha kwa Wanachama wa kaunti.
Pia ameomba kaunti kupunguza vikwazo vya barabara ambavyo vinazuia usafirishaji wa bidhaa kutoka bandari ya Mombasa kwenda nchi nyingine za Afrika Mashariki.
amesema Kenya inapoteza biashara yake ya kikanda kwa nchi jirani kwa sababu ya changamoto zinazozuia usafirishaji wa haraka wa bidhaa.
Mauzo ya nje ya Kenya imefikia asilimia 25 ya bidhaa na huduma kwa nchi za Afrika Mashariki na hii imebakia soko muhimu zaidi kwa mauzo ya nje ya Kenya.
Katibu wa kudumu Susan Koech amesema serikali itasaidia wilaya za mpaka ili kuhakikisha kuwa maono ya Jumuiya ya Afrika Mashirika EAC yameonekana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |